Jumamosi 11 Oktoba 2025 - 22:15
Tunataraji kushuhudia uundwaji wa taifa la Palestina

Hawza/ Rais wa Kolombia amepongeza makubaliano kati ya Israel na Hamas kuhusu awamu ya kwanza ya mpango wa amani katika Ukanda wa Ghaza, akieleza matumaini yake kwamba usitishaji huu wa mapigano utakuwa utangulizi wa kuundwa kwa dola huru ya Palestina.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza Gustavo Petro, Rais wa Kolombia, aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii X:
“Pamoja na wananchi wa Palestina, tunafurahia usitishaji mpya wa mapigano. Tunajua kwamba hapo awali usitishaji mwingi haukutoa matokeo, lakini tunatumai safari hii tutaweza kupiga hatua kuelekea kuundwa kwa taifa huru la Palestina.”

Petro, ambaye anajulikana kuwa mkosoaji mkali wa uvamizi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza, akirejelea nafasi ya Marekani katika mzozo huo, alisema:


“Trump alikuwa na ufunguo wa suluhisho la mzozo huu mikononi mwake, na safari hii ameutumia kwa usahihi. Bila msaada wa kijeshi kutoka Marekani, Netanyahu asingeweza kuendelea na uvamizi wake.”

Aidha, alisisitiza kwa kusema:

“Kadiri Trump alivyoendelea kumuunga mkono Netanyahu, mauaji ya halaiki huko Ghaza yasingeweza kukoma. Lakini shinikizo la mataifa, upatanishi wa Qatar na Misri, pamoja na misimamo thabiti ya nchi kama Afrika Kusini na Kolombia, viliweza kuleta mwanya, ingawa mdogo, kati ya Ikulu ya White House na Tel Aviv.”

Rais wa Kolombia alikumbusha kwamba katika hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alipendekeza kuundwa kwa ‘jeshi la uokozi’ kwa ajili ya kusaidia Palestina, na akaongeza:
“Ikiwa haki ya kujitawala kwa taifa la Palestina itaheshimiwa, mpango huo utabaki hai, lakini jukumu lake litakuwa ni kujenga upya na kushirikiana bega kwa bega na wananchi wa Palestina.”

Kwa mujibu wa mpango uliowasilishwa kwa ubunifu wa Donald Trump na kupitia upatanishi wa Qatar, Misri, na Uturuki, utawala wa Kizayuni unalazimika kusitisha mashambulizi yake dhidi ya Ghaza, na kwa kubadilishana na kuachiwa kwa maelfu ya wafungwa wa Kipalestina, mateka wote — walio hai na waliokufa — watatolewa huru ndani ya masaa 72.

Kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa Israel, kati ya mateka 48 wa Kiyahudi, akriban ni watu 20 pekee walio hai. Miongoni mwao yupo Elkana Buhbot, raia mwenye uraia pacha wa Kolombia na Israel, ambaye mkewe ni Mkikolombia na ni baba wa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha